HIVI PUNDE>>>
Loading...

Monday, May 28, 2018

Rais Na Mwenyekiti Wa CCM Dr Magufuli Aongonza Mkutano Wa Halmashauri Kuu Ya Taifa (NEC) Ya CCM Jijini Dar Es Salaam Leo


Rais wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Dkt. John Pombe Magufuli  akiwa meza kuu katika Ukumbi wa mikutano wa Kikwete katika Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ukumbi wa Kikwete leo Jumatatu Mei 28, 2018  

Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahman Kinana wakati akisoma muhtasari wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Katika ukumbi wa Kikwete jijini Dar es salaam leo Jumatatu Mei 28, 2018
Wajumbe wakishangilia baada ya  Rais wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Dkt. John Pombe Magufuli kuwaita  Ndg. Mizengo Pinda na Ndg. Makongoro Nyerere waingie ukumbini baada ya kukubaliwa kuwa wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) wa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika ukumbi wa Kikwete jijini Dar es salaam leo Jumatatu Mei 28, 2018
Read More

Uwoya Aelezea Jinsi Mwezi Mtukufu Unavyodumisha Penzi Lake na Dogo Janja


Mwanadada Irene Uwoya na mume wake Dogo Janja amabao kila siku hawaishiwi na drama katika  mitandao wanakuja tena kivingine na kuelezea jinsi mwezi mtukufu wa Ramadhani unavyodumisha mahusiano katika ndoa yao.

Irene anasema kuwa akiwa kama mke halali wa Abdul (janjaro) anahaki zote za kukaa na kutulia kipindi hiki cha ramadhan na kumpikia mume wake  kwa sababu hicho ni kitu alichozoea hata katika ndoa yake iliyopita.
 
"Kuhusu kufunga kwa upande wangu nilishazoea kwa sababu hata siku za nyuma za ramadhani nilikuwa nikifanya hivyo hivyo nilipokuwa na Ndiku na kwa sababu sasa hiv mimi ni mke halali kabisa wa Abdul basi nina haki ya kutulia na kumpikia mume wangu futari."-Uwoya
Read More

Vilio Vyatawala Bungeni....Bunge Laahirishwa Hadi Kesho


Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson leo asubuhi ameahirisha Bunge mpaka kesho saa tatu asubuhi kupisha maombolezo ya kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Buyungu Mwl. Kasuku Bilago aliyefariki siku ya Jumamosi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
 Vilio na simanzi vilitawala katika ukumbi wa Bunge kutokana na kifo hicho cha Mbunge huyo wa Chadema aliyefariki dunia Jumamosi Mei 26. 

“Waheshimiwa wabunge, Spika wa Bunge mheshimiwa Job Ndugai  anasikitika kuwatangazia kifo cha mbunge wa Buyungu, Kasuku Bilago kilichotokea juzi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, kwa mujibu wa kanuni zetu, leo shughuli za Bunge hazita endelea na badala yake tutakuwa na maombolezo,” amesema Naibu Spika.

Wakati Naibu Spika Ackson akitoa taarifa za msiba na kuahirisha Bunge, wabunge Julius Kalanga (Monduli), Suzan Kiwanga (Mlimba), Halima Mdee (Kawe) na Dk Semesi Sware (Viti Maalum ) wote wa Chadema walikuwa wakilia.

Mbunge wa Bunda, Ester Bulaya (Chadema) alishindwa kabisa kujizuia na wabunge walilazimika kumpa usaidizi.

Naibu Spika Dkt. Tulia amesema kuwa Wabunge watakao kwenda kuwakilisha kwenye mazishi hayo wataondoka Dodoma siku ya Jumanne asubuhi na kurejea Dodoma Jumatano mara baada ya mazishi hayo kumalizika.

Pamoja na hayo, Naibu Spika ameendelea kwa kusema "siku ya kesho tutakuwa na kikao cha Bunge kama kawaida isipokuwa tutahairisha Bunge saa sita mchana ili kutoa fursa kwa shughuli za heshima za mwisho kwa mwili wa marehumu Bilago na baada ya hapo tutaendelea na maombelezo hadi siku ya Jumatano".
Read More

ACT Wazalendo Wahoji Matumizi Fedha Za Korosho


Chama cha ACT Wazalendo kimeitaka Serikali kupeleka haraka asilimia 65 ya fedha za mauzo ya nje ya korosho ghafi kwa Bodi ya Korosho ili zitumike kama zilivyokusudiwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano ya Umma wa chama hicho, Ado Shaibu, alisema kutokupeleka fedha hizo kutasababisha gharama za uzalishaji kwa wakulima kuongezeka kutokana na ununuaji wa pembejeo kutegemea kwa asilimia 100 katika fedha hizo.

Alisema jambo hilo lilitokea mwaka jana kupanda kwa dawa aina ya salfa (Sulphur) katika maeneo mengi kutoka Sh 16,000 hadi kufika Sh 70,000.

“Kwa mujibu wa sheria ya korosho namba 18 ya mwaka 2009 kifungu 17(A), inaitaka Serikali kuingiza fedha hizo Bodi ya Korosho lakini fedha hizo hazijapelekwa kwa miaka miwili sasa,” alisema Shaibu.

Alisema hata hivyo kwa mujibu wa taarifa ya Bodi ya Korosho iliyotolewa na kamati ya Bunge ya Maji, Kilimo na Mifugo kwa misimu miwili ya mauzo ya korosho, bodi haijapokea fedha hizo na hivyo kuleta athari mbalimbali katika kilimo hicho.

Aliongeza kuwa taarifa hiyo inadai kuwa Bodi ya Korosho haijapokea Sh bilioni 211 ambapo kwa mwaka wa fedha wa 2016/17 wanadai Sh bilioni 91 na 2017/18 wanadai Sh bilioni 110.

“Kutopeleka fedha hizi kutaathiri Kituo cha Utafiti cha Naliendele kinachozalisha mbegu bora za korosho na dawa za kudhibiti magonjwa ambacho kinategemea fedha hizo kwa asilimia 90 kujiendesha kitashindwa kufanya kazi zake kwa ufanisi,” alisema Shaibu.

Aliongeza kuwa athari nyingine ni kuvurugika kwa mfumo wa stakabadhi ghalani kwa sababu ya usimamizi wa mfuko huo kutegemea fedha hizo kwa asilimia 100.

“Mafunzo ya kilimo bora kwa wakulima na maofisa ugani yamesimama kwa sasa kutokana na kukosekana kwa fedha hizo,” alisema Shaibu.

Alisema wanamwomba Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, kulitolea ufafanuzi suala hili ili kuondoa mkanganyiko unaojitokeza.

Akizungumzia kuhusu uchaguzi wa ndani ya chama hicho, Shaibu, alisema umefikia hatua ya majimbo na kitaifa utafanyika Agosti 25 hadi 27, mwaka huu jijini Mbeya.

Alisema chama hicho kinapinga kauli ya Waziri wa Mambo ya Nje, Balozi Augustine Mahiga, aliyoitoa hivi karibuni bungeni kuwa suala la uanachama wa Sahara Magharibi lina utata wa kisheria katika Umoja wa Afrika na katika duru za kimataifa.

“Tunapinga kauli hii kwa kuwa Tanzania tumekuwa mstari wa mbele kuwasaidia kupata uhuru wa Sahara Magharibi chini ya chama cha ukombozi cha Polisalio,” alisema Shaibu.

Akizungumza hivi karibuni, Waziri Mahiga, alisema Polisalio ni chama cha ukombozi kilichopewa hadhi ya Serikali na uanachama wa Umoja wa Afrika tangu 1982, lakini suala hilo limeanza kuleta utata kisheria.
Read More

Baada Ya Diamond, Lynn Ahamishia Majeshi Yake Kwa Chris Brown


Video vixen Irene Hillary maarufu kama Lynn aliyejizolea umaarufu Kupitia video ya Rayvanny ya wimbo wa ‘Kwetu’ amefunguka kuhusu mahaba mazito kwa supastaa wa kimataifa

Lynn alipata umaarufu baada ya kudaiwa kutoka kimapenzi na staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz hadi kubeba mimba yake.

Lakini hivi sasa Lynn ameweka wazi kuwa mapenzi yake yote yamehamia kwa staa wa Muziki kutoka Marekani Chris Brown na kusema Staa Huyo anamkosesha usingizi akimuwaza.

Kwenye mahojiano na Risasi Jumamosi, Lynn alisema kuwa ametokea kumpenda sana mwanamuziki huyo kiasi ambacho haelewi atafanyaje ila anaomba katika maisha yake siku moja akutane naye, amueleze hisia zake.

“Hivi ulishawahi kumpenda mtu mpaka ukawa huelewi sababu? Sasa ndio mimi nilivyo kwa Chris, naamini siku nitaonana naye na kama ikitokea hivyo kwa kweli nitamfikishia hisia zangu, kama atakubali au kukataa, niwe tu nimemuambia, naamini nitakuwa na amani”.
Read More

Korea Kaskazini Yasisitiza Ipo Tayari Kwa Mazungumzo na Marekani


Ni nia ya kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un kuwa mkutano kati yake na Rais wa Marekani Donald Trump uendelee, imeeleza taarifa ya vyombo vya habari vya Korea Kaskazini.

Hii ni kutokana na mkutano wa kushtukiza wa siku ya Jumamosi kati ya Kim na Rais wa Korea Kusini, Moon Jae-in.

Rais Trump alisitisha mkutano uliopangwa kufanyika tarehe 12 mwezi Juni kuzungumzia mpango wa nuklia wa Korea Kaskazini, lakini alisema Jumamosi kuwa mambo yanaendelea vizuri sana

Wakati huo huo ujumbe wa Marekani uliripotiwa kwenda Korea Kaskazini siku ya Jumapili.

Balozi wa zamani wa Marekani nchini Korea Kusini, Sung Kim, atafanya mazungumzo na naibu waziri wa mambo ya nje wa Korea Kaskazini kuhusu maandalizi ya mkutano, vyombo vya habari vya Marekani na Korea Kusini vimeeleza.

Mkutano huo ni matunda ya jitihada za kidiplomasia ambazo zilianza mwaka huu kujaribu kuondoa hali ya msuguano uliohofiwa kugeuka kuwa makabiliano ya kijeshi kati ya Korea Kaskazini, Korea Kusini, na Marekani.
Credit:BBC
Read More

Mwanafunzi Chuo cha SAUT Ajinyonga Baada ya Timu Yake ya Liverpol Kufungwa


Mwanafunzi wa mwaka wa pili Chuo kikuu cha ‘St. Augustine’ kampasi ya Mbeya Moses Mashaka amejinyonga mara baadaya timu yake ya Liverpol kushindwa kutwaa ubingwa wa klabu bingwa barani ulaya.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Jijini Mbeya Naibu Kamishna wa Polisi Mussa Taib amesema Moses (24) amejinyonga mara baadaya ‘kubet’ na timu yake kushindwa kutwaa ubingwa.

“Mwanafunzi wa chuo kikuu cha sauti mwaka wa pili anachukua shahada ya ualimu amefariki baada ya ‘kubet’ pesa ambazo hazijulikani ni kiasi gani na baadaya Liverpol kushindwa ndipo akachukua uamuzi huo”,amesema kamanda Taibu.

Aidha Kamanda Taibu amewataka wanafunzi kuacha kutumia fedha za wazazi kwa mambo yasiyohusiana na masuala mazima ya elimu, kwani matokeo yake ni hasara kwa wazazi.
Read More

Sunday, May 27, 2018

Lema alipongeza Bunge, akomaa na Stahiki za Tundu Lissu


Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amefunguka kuwa bado wanaendelea kutafakari suala la Mbunge wa Sigida Mashariki Tundu Lissu kuhangaika na kutafuta misaada ya matibabu kwa watu mbalimbali duniani, kwani Bunge bado linatafakari kuhusu stahiki zake, haki na gharama za matibabu.

Mhe. Lema amezungumzia hayo ikiwa ni siku moja tangu kutokea kwa kifo cha Mbunge wa Buyungu, Kasuku Bilago aliyefariki wakati akipatiawa matibabu katika hospitali ya Taifa, Muhimbili.

Lema amesema "Mwili wa Marehemu Mhe. Bilago umepata heshima, haki na stahiki ya Kibunge, tumefanya kikao tena Kati ya Bunge, Chama na Familia, wema wa Bunge kwa mwili wa marehemu umekuwa ni wa kifani".

Ameongeza "Wakati tunalishukuru Bunge kwa wema huu, bado tunaendelea kulitafakari la rafiki yetu Lissu aliyeko Ubeligiji".

Lissu ambaye anatibiwa nchini Ubelgiji alipigwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 9, 2017 maeneo ya Area D akiwa anatokea katika majukumu yake ya kikazi bungeni Dodoma.

Sababu za Lissu kutotibiwa na Bunge ziliwekwa wazi na Spika wa Bunge, Job Ndugai  siku moja baada ya tukio hilo ambapo alisema kuwa utaratibu wa matibabu kwa mbunge ulikuwa umeshafuatwa lakini familia pamoja na chama  waliamua kumpeleka Nairobi, na siyo kama wao walishindwa kumpeleka nchini India.
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amefunguka kuwa bado wanaendelea kutafakari suala la Mbunge wa Sigida Mashariki Tundu Lissu kuhangaika na kutafuta misaada ya matibabu kwa watu mbalimbali duniani, kwani Bunge bado linatafakari kuhusu stahiki zake, haki na gharama za matibabu. Mhe. Lema amezungumzia hayo ikiwa ni siku moja tangu kutokea kwa kifo cha Mbunge wa Buyungu, Kasuku Bilago aliyefariki wakati akipatiawa matibabu katika hospitali ya Taifa, Muhimbili. Lema amesema "Mwili wa Marehemu Mhe. Bilago umepata heshima, haki na stahiki ya Kibunge, tumefanya kikao tena Kati ya Bunge, Chama na Familia, wema wa Bunge kwa mwili wa marehemu umekuwa ni wa kifani". Ameongeza "Wakati tunalishukuru Bunge kwa wema huu, bado tunaendelea kulitafakari la rafiki yetu Lissu aliyeko Ubeligiji". Lissu ambaye anatibiwa nchini Ubelgiji alipigwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 9, 2017 maeneo ya Area D akiwa anatokea katika majukumu yake ya kikazi bungeni Dodoma. Sababu za Lissu kutotibiwa na Bunge ziliwekwa wazi na Spika wa Bunge, Job Ndugai siku moja baada ya tukio hilo ambapo alisema kuwa utaratibu wa matibabu kwa mbunge ulikuwa umeshafuatwa lakini familia pamoja na chama waliamua kumpeleka Nairobi, na siyo kama wao walishindwa kumpeleka nchini India.
Read More

Mtanzania Aibuka Kidedea Mashindano Ya Kuhifadhi Quran Afrika.....Waziri Mkuu amtaka Sheikh Kishki akaonane na Waziri wa Ardhi atoe maamuzi ya kiwanja


KIJANA wa Kitanzania, Shujaa Suleiman Shujaa ameibuka kidedea na kitita cha sh. milioni 15 katika mashindano ya 19 ya Afrika ya kuhifadhi Quran kwenye kundi la washiriki wa juzuu 30.

Shujaa mwenye miaka 23 ambaye ni mkazi wa Morogoro, amejishindia pia laptop, kiwanja chenye hati eneo la Kigamboni kilichotolewa na kampuni ya Property International ya jijini Dar es Salaam pamoja na dola za Marekani 500 kutoka kwa Bw. Ahmed Seif “Magari” aliyetoa dola 500 kwa washindi wote watano.

Akizungumza na maelfu ya waumini na Watanzania waliofurika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jana  mchana (Jumapili, Mei 27, 2018), Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka Watanzania waendelee kuilinda amani iliyopo nchini kwani ikipotea hakuna atakayeweza kufanya ibada.

“Mtakubaliana nami kuwa amani ya nchi yetu, ndiyo inatufanya tutembee vifua mbele dhidi ya wenzetu, ni neema kubwa ambayo kila muumini anapaswa kuilinda kwani ikipotea hata mkusanyiko wetu huu wa leo si rahisi kufanyika mahali kama hapa,” alisema.

“Leo hii tuko hapa uwanjani kwa sababu tuna amani, kama Serikali isingekuwa inashirikisha Watanzania wote kulinda amani, basi tusingeweza kukutanika hapa. Kuna nchi 18 ziko hapa, na watu wake wamekuja hapa uwanjani kwa kuwa wana uhakika na amani tuliyonayo sisi Watanzania,” alisema.

Alisema katika nchi ambazo amani imetoweka, watu wanalazimika kufanya shughuli za ibada majumbani au kwa kujificha. 
“Wenzetu hao, hawapati fursa adhimu kama hii ya kujumuika pamoja na majirani, ndugu, jamaa na marafiki kusikiliza na kufurahia kisomo cha Quran au kufanya shughuli nyingine za kiuchumi na kijamii,” aliongeza.

Aliwataka Watanzania waendelee kubeza na kupuuza kauli za walio wachache ambao kwao kuzungumzia amani ni kujipendekeza kwa Serikali. “Watu hao wamesahau kwamba tofauti katika Uislamu hazikuanza leo, lakini tofauti hizo hazikuwa sababu ya wema waliotangulia kuacha kuheshimiana na kushirikiana,” alisisitiza.

Mshindi wa pili kwenye kundi hilo la juzuu 30 ni Ahmed Noor wa Sudan ambaye ameshinda sh. 12,564,750 pamoja na laptop akifuatiwa na Muzamil Awadh Mohamed wa Sudan alijishindia sh. milion 7.5 pamoja na laptop zilizotolewa na kampuni ya Camara Education.

Mshindi wa nne ni Abdulally A. Mohammed wa Kenya aliyepata zawadi ya sh. 5,711,000 na wa tano ni Ibrahim Maazur kutoka Niger, aliyepata sh. 3,426,000. Washindi hao wote watano walipewa zawadi ya kwenda hijja na Waziri wa Mambo ya Dini wa Saudi Arabia, Dk. Saleh Ally Sheikh.

Washiriki wengine kwenye kundi la juzuu 30 walitoka nchi za Rwanda, Burundi, Msumbiji Djibouti, Kenya, Ethiopia, Congo DRC, Nigeria, Ghana na Afrika Kusini.

Washiriki wengine waliopewa zawadi ni wale walioweza kuhifadhi Juzuu tatu (washindi watatu), Juzuu tano (washindi watatu); Juzuu 10 (washindi watatu) na Juzuu 20 (washindi watatu).

Viongozi wengine waliohudhuria mashindano hayo ni Makamu wa Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Dk. Mohammed Gharib Billal, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa Tanzania kutoka Saudi Arabia, Comoro, Oman, Uturuki, Kenya, Msumbiji na Nigeria, Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir bin Ally na Rais wa taasisi ya Al-Hikma, Sheikh Sharif Abdilkadir Al-Ahdal.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amemtaka Sheikh Nurdin Mohammed Ahmad (maarufu kama Sheikh Kishki) akaonane na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bw. William Lukuvi ili atoe maamuzi ya kiwanja chao kilichopo eneo la Matumbi ambacho mwaka jana aliagiza kifuatiliwe taratibu zake na kisha wapatiwe.

“Kuhusiana na suala la kiwanja mlichosema, mamlaka ya awali ni Manispaa ya Temeke na ilishakamilisha taratibu zote za kisheria, ikapeleka kwa Afisa Ardhi wa Mkoa kuona kama limepita kwenye vikao vyote ndipo wanaenda wizarani kupata kibali. Hakuna sababu ya wizara kuikatalia manispaa huku eneo lenyewe likiwa kwenye ramani kuu ya manispaa yenyewe, nenda mumuone Waziri mwenye dhamana, awape ardhi,” alisema.

Waziri Mkuu amefikia hatua hiyo baada ya kupewa taarifa akiwa jukwaani kwamba taasisi ya Al-Hikma iliwasiliana na Manispaa ya Temeke, hadi mkoani wakapewa barua zinaonyesha eneo liko sawa lakini walipofika wizarani wamekwamishwa na Afisa mmoja aliyemtaja kwa jina moja la Mama Mpetula.

Juni 11, mwaka jana katika mashindanio ya 18, taasisi ya Al-Hikma waliomba wapatiwe kiwanja na.118 kwenye kitalu E kilichoshikamana na kiwanja na. 117 chenye shule yao ya Al-Hikma Girls iliyoko Temeke ili waweze kujenga zahanati.
Read More

Taarifa Kwa Umma Kuhusu Mazishi Ya Aliyekuwa Mbunge Wa Jimbo La Buyunga,marehemu Mwl.kasuku Samson Bilago


Read More

PICHA: Rais Magufuli Alivyokutana na Kufanya Mazungumzo na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 27 Mei, 2018 amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahman Kinana, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Katika mazungumzo hayo Mhe. Rais Magufuli alipokea salamu kutoka kwa viongozi wa chama na Serikali wa Afrika Kusini na Zimbabwe ambako hivi karibuni Ndg. Kinana aliongoza ujumbe wa viongozi wa CCM kutembelea nchi hizo na kukutana na viongozi wakuu wa vyama tawala vya ANC na ZANU-PF vinavyoongoza Serikali.

Aidha, Mhe. Rais Magufuli na Ndg. Kinana wamezungumzia maandalizi ya vikao vya Kamati Kuu ya CCM (CC) na Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) vitakavyofanyika  tarehe 28-29, Mei, 2018 Jijini Dar es Salaam.
Read More

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya May 28


Read More

Saturday, May 26, 2018

Kamanda Mambosasa Azungumzia 'Mabilioni ya Dr Shika'


Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam Lazaro Mambosasa amesema swala la Dk. shika kuingiza pesa zake Tanzania hana uhakika nalo na mtu kutumiwa hela kihalali si kosa 
Amesema kuwa kama taarifa hizo ni za uongo anaweza kupuuzwa ila endapo kauli yake italeta madhara basi hatua zitachukuliwa.

Mambosasa amezungumza hayo leo pindi alipokuwa anaongea na waandishi wa habari akitoa ripoti za jeshi la polisi kuwashikilia watuhumiwa mbambali kwa kufanya makosa ya unyang’anyi kwa kutumia silaha za moto.

”Mtu kutumiwa hela kama ni halali haziingii kwenye pesa ambazo zinatakatishwa au hela ambazo zinapatikana kwa njia isiyo halali si kosa lakini kama ni muongo tu anajisema basi kuna mawili anaweza kupuuzwa lakini kama kauli zake zitamwaathiri yeyote anaweza kuja kulalamika na jeshi la polisi likachukua hatua” amesema Mambosasa.

Mambosasa amezungumza hayo pindi alipokuwa anajibu swali la mmoja wa waandishi wa habari baada ya kuhoji juu ya uhalali wa pesa za Dk. Luis Shika ambaye hivi karibuni taarifa zimeeleza tayari ameingiza mabilioni yake ya fedha nchini Tanzania.

Siku chache zilizopita Dkt. Louis Shika alivieleza baadhi ya vyombo vya habari nchini juu ya ujio wa fedha zake na baadhi ya vipande vya dhahabu zilizokuwa nje ya nchi kuwa tayari zimewasili nchini kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (JKNIA) na kupelekwa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) kwa ajili ya kuhakikiwa.

Taarifa hizo zilizua mjadala mkubwa mtandaoni ambapo watu walionesha kutokuamini kwa ujio huo wa pesa za  Dk. Shika wakidhani ni stori zisizo na ukweli ndani yake.

Hata hivyo Shika alithibitisha ujio wa mali hizo na kuonyesha baadhi ya nyaraka zinazothibitisha umiliki wa mali hizo.
Read More

Mo Salah atacheza World Cup? Daktari wa timu atoa neno hili.


Mtanange wa yule Bingwa wa Ulaya umekamilika. Real Madrid wameshinda taji lao la tatu mfululizo kwa ushindi wa mabao matatu kwa moja. Golikipa wa Liverpool Karius akisababisha uzembe ulioigharimu timu hao baada ya kurusha mpira kimakosa na ukagomga Benzema aliyegfunga bao la kwanza kabla ya Mane kusawazisha. unga magoli mawili. Bale alitokea benchi na kufunga mabao mawili.

Niliwahi kusema kinyago cha Gazzaniga (Kombe la Dunia) kiliwanyima mastaa wengi usingizi. Majeraha ilikuwa changamoto kubwa sana kwa wachezaji wa pande zote.
kilichotokea leo ni kitu ambacho wengi tulitarajia kutapoteza ladha ya mchezo huu.

Mo Salah ambaye alikuwa mchezaji tegemezi wa Liverpool hivi leo atolewa kwenye mchezo mapema kabisa baada ya kuumia bega. Ilikuwa ni kashkash kati yake yeye na Sergio Ramos. Ramos alikwenda kumkaba Salah na ilionekana wakishikana mkono. Picha na video zinaonesha kuwa alimvuta mkono na kumsababisha Salah kuondoka vibaya na kulalia bega lake.

Je wachambuzi wakubwa wanasemaje?
Rio Ferdinand
Ramos amekaba vyema. Alifanya kitu ambacho mlinzi yeyote angefanya. Sidhani kama alidhamiria.
Frank Lampard
mnapokuwa mmesogeleana sana mara nyingi ni rahisi sana kushikana mikono. ile ni bahati mbaya sana.

Rio na Lampard hawa ni waingereza na wana haki ya kutoa Maoni yao. Jana nilimsikia David Beckham aliweka pembeni sana suala la Uzalendo. Na aliweka mapenzi yake dhahiri kuwa Real inafaa iifunge Liverpool. Rio nae ni hasimu mkubwa wa Liverpool. Bila shaka ukiangalia ile video utagundua hakuna ajali. kuna tofauti kubwa ya kushikana na kumvuta mtu kwa makusudi ukidhamiria.

John Simpson anasema hivi
Nimeangalia maoni ya wachambuzi wakubwa, wanasema lile tukio ni ajali. Sawa. Lakini ukimwangalia Ramos wakati Salah anatolewa nje utagundua alidhamiria.

kuna baadhi ya video zinamuonesha Ramos akitabasamu na Mwamuzi wa pembeni.
David Maddock anasema
Inauma sana. Ramos amefanya kitendo cha kikatili haswa. Hajaharibu tu ndoto za Salah za Uefa pia huenda ameharibu ndoto wa Wamisiri wote.

Mo Salah taarifa zinasema mishipa ya bega imeachana. Na majibu kamili yatatolewa wakirudi jijini Liverpool. Hii inaleta wasiwasi mkubwa kama atahitaji kufanyiwa upasuaji. na itamlazimu kukosa michuano ya kombe la dunia.

hata hivyo taarifa za hivi punde zinasema kuwa ukurasa wa timu ya taifa ya Misri umeweka taarifa kuwa Mo Salah atacheza michuano ya kombe la dunia
Read More